Uliza Sheria

Pata Elimu Na Msaada Wa Kisheria

Kwa Huduma Za Kisheria Mawasiliano
0713 888 040

Kuhusu Sisi

Uliza Sheria imekuja kama suluhisho la matatizo mbali mbali ya kisheria yanayoikumba jamii yetu. Taaluma ya sheria ni moja ya taaluma muhimu sana katika ustawi wa jamii yoyote ya kistaarabu. Ni muhimu sana jamii ikafahamu mambo ya msingi yanayohusu wajibu na haki zao.

Ulizasheria inakuja kama jibu katika changamoto na maswali yanayoikumba jamii yetu.

Lengo kuu la mtandao huu;

  • Kutoa elimu ya msingi ya sheria kwa mwananchi wa kawaida kabisa ili apate kufahamu namna ya kuishi kwa mujibu wa sheria
  • Kutatua matatizo na kutoa majibu ya maswali ya jamii katika changamoto za kisheria wanazokumbana nazo kila siku.
  • Kusaidia lengo la Taifa 2025 kuwa nchi yenye kuzingatia sheria na utawala bora.

Katika blog yetu ya ulizasheria utakutana na makala nzuri za kisheria zinazokupa mwongozo katika maeneo mbalimbali ya kimaisha, uchambuzi wa sheria mbalimbali, sehemu ya maswali na majibu, uchambuzi wa kesi n.k.

Ulizasheria inakuja kama suluhu ya kumwezesha msomaji kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za kisheria yeye mwenyewe.