SISI NI NANI?
Uliza Sheria imekuja kama suluhisho la matatizo mbali mbali ya kisheria yanayoikumba jamii yetu. Taaluma ya sheria ni moja ya taaluma muhimu sana katika ustawi wa jamii yoyote ya kistaarabu. Ni muhimu sana jamii ikafahamu mambo ya msingi yanayohusu wajibu na haki zao. Uliza Sheria inakuja kama jibu katika changamoto na maswali yanayoikumba jamii yetu.