Karibu Kwenye Mtandao Wa Uliza Sheria

Uliza Sheria imekuja kama suluhisho la matatizo mbali mbali ya kisheria yanayoikumba jamii yetu. Taaluma ya sheria ni moja ya taaluma muhimu sana katika ustawi wa jamii yoyote ya kistaarabu. Ni muhimu sana jamii ikafahamu mambo ya msingi yanayohusu wajibu na haki zao.

Uliza Sheria inakuja kama jibu katika changamoto na maswali yanayoikumba jamii yetu.

Lengo kuu la mtandao huu;

  • Kutoa elimu ya msingi ya sheria kwa mwananchi wa kawaida kabisa ili apate kufahamu namna ya kuishi kwa mujibu wa sheria
  • Kutatua matatizo na kutoa majibu ya maswali ya jamii katika changamoto za kisheria wanazokumbana nazo kila siku.
  • Kusaidia lengo la Taifa 2025 kuwa nchi yenye kuzingatia sheria na utawala bora.

Katika blog yetu ya ulizasheria utakutana na makala nzuri za kisheria zinazokupa mwongozo katika maeneo mbalimbali ya kimaisha, uchambuzi wa sheria mbalimbali, sehemu ya maswali na majibu, uchambuzi wa kesi n.k.

Ulizasheria inakuja kama suluhu ya kumwezesha msomaji kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za kisheria yeye mwenyewe.

Huduma za Uliza Sheria

Katika blog ya ulizasheria utakutana na huduma kadhaa;

  • Ushauri wa kisheria katika maeneo mbali mbali mfano ardhi, kazi, mirathi, ndoa, jinai na madai.
  • Uandishi wa nyaraka za kisheria, mfano mikataba, wosia, nyaraka za uanzishaji Kampuni n.k.
  • Usimamizi/uwakilishi wa kesi mahakamani au mabaraza
  • Kutoa elimu ya kisheria
  • Kutoa mafunzo kwa semina, makongamano, warsha kwa wadau wa sheria
  • Kushuhudia nyaraka za kisheria (attestation and certification of documents)
  • Kusimamia usajili wa kisheria kwenye Taasisi za Umma, mfano BRELA, Manispaa, RITA n.k
  • Wakala wa kuuza au kununua vitu (real estate broker)

 

Mtandao huu unaendeshwa na Isaack Zake ambaye ni  wakili wa kujitegemea tangu 2011 na Mwanzilishi wa Ofisi ya Wakili inayoitwa Zake Advocates. Isaack Zake amekuwa akishugulika na ushauri wa kisheria, uandishi wa nyaraka mbali mbali za kisheria na usimamizi wa kesi katika mahakama, mabaraza ya Ardhi na Nyumba na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.

Karibu sana ujifunze na kupata huduma za kisheria.

2 replies

Comments are closed.