Nafasi ya Mtoto wa Nje ya Ndoa katika Mirathi -2

Utangulizi

Karibu sana ndugu msomaji na mfuatiliaji wa ukurasa huu  kwenye mtandao wako wa Uliza Sheria. Kama kawaida yetu lengo la kukuletea makala hizi fupi ni kukusaidia kuishi kwa mujibu wa sheria kila siku. Leo tunaendelea kujifunza na mfululizo wa makala zinazohusu masuala ya mirathi. Karibu tujifunze kwa pamoja.

Historia ya Nafasi ya Mtoto wa nje ya Ndoa katika Mirathi

Katika makala iliyopita tuliweza kuona kwa utangulizi juu ya Nafasi ya mtoto wa nje ya ndoa katika mirathi. Tumeona jinsi historia ya kisheria kupitia mirathi zinazofuata dini au mila suala la mtoto wa nje limekuwa na changamoto kubwa kwa kukosa urithi kwa baba yake. Mtoto wa nje aliweza tu kuhesabiwa mrithi kwa upande wa mirathi ya mama yake.

Mtazamo wa Sheria baada ya mwaka 2009

Mwaka 2009 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria maalum ya mtoto. Sheria hii ilianza kutumika mwaka 2009. Sheria hii haikuleta tu mabadiliko makubwa juu ya masuala ya mtoto katika jamii bali ilikwenda mbali kuathiri na masuala ya mirathi au haki ya mtoto kurithi.

Kupitia Sheria ya Mtoto ya 2009 tumeweza kuona haki mbalimbali za mtoto zilizoainishwa ikiwepo na haki ya kurithi mali kutoka kwa wazazi wake iwe ni baba au mama. Sheria hii imeondoa ubaguzi ambao watoto wa nje ya ndoa ambao walizoeleka kuwa ni watoto haramu katika jamii kubainishwa haki zao na kuhesabiwa katika mirathi ya wazazi wao bila kujali kuwa walizaliwa ndani au nje ya ndoa.

Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mtoto ya 2009 inaeleza wazi kuwa ‘mtu hatoruhusiwa kumnyima mtoto haki ya kufurahia au kutumia mali ya mzazi wake’

‘A person shall not deprive a child of reasonable enjoyment out of the estate of a parent’ S.10 of Law of Child Act

Kwa mtazamo huu wa kisheria mtoto yeyote anayo haki ya kurithi mali ya mzazi wake ikiwa ni baba au mama yake pasipo ubaguzi wowote ule. Mtazamo huu wa sheria ya Mtoto ya 2009 unaendana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inayoeleza kwenye Ibara ya 12 inayosema;

‘Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa’

Pia Sheria ya Mtoto Kifungu cha 3 kinaeleza wazi kuwa mtoto hapaswi kubaguliwa kwa namna yoyote ile kwa misingi ya jinsia, rangi, umri, dini, lugha, mtazamo wa kisiasa, hali ya afya yake, mila zake au kabila lake, malali alipotoka, kuzaliwa kwake, hali yake ya kijamii na kiuchumi au kwa hadhi yake yoyote ile.

Kwa msingi huu tunaona wazi kuwa Sheria zote za kimila au kidini ambazo zilikuwa hazimtambui mtoto wa nje ya ndoa kama mrithi halali wa mzazi wake wa kiume yaani baba hazina tena nguvu.

Hivyo katika mazingira haya ni muhimu sana kwa wazazi kuzingatia juu ya watoto na kuwatambulisha kwa ndugu au wenzi wao ili kuondoa migongano isiyo ya lazima. Baba kama umepata mtoto wa nje ya ndoa fanya utaratibu mapema wa kutoa taarifa naye aweze kujua kwani usipofanya hivyo baada ya muda utaisababishia familia mgogoro mkubwa kwani mtoto huyo ana haki ya kudai urithi kwa baba yake mzazi.

Muhimu zaidi kuzingatia mtoto huyu endapo hajatambulishwa kwa familia yake na kifo cha baba yake kimetokea zipo njia za kisanyansi kwa siku hizi kuweza kutambua endapo ni kweli mtoto wa marehemu, Mahakama inaweza kuamuru upimaji wa vinasaba yaani DNA kutambua uhusiano wa mtoto na marehemu kupitia ndugu wengine.

Hitimisho

Leo tumeangalia tena Nafasi ya Mtoto wa Nje ya Ndoa katika Mirathi kwa kuitazama Sheria ya Mtoto ya 2009 na athari chanya ilizozileta kwenye jamii. Kazi muhimu ni kuhakikisha wazazi wanatambua watoto wao na wenzi walio na watoto wa nje pia kuwatambulisha. Nisisitize tatizo hili halipo tu kwa wanaume bali hata wanawake katika jamii wamekuwa wakiwabambikia waume zao watoto wa nje ya ndoa na mzazi wa kiume anajikuta mirathi yake inaenda kwa mtoto asiye wake. Hii ni changamoto kubwa katika jamii lakini inatupasa kuikabili kwa pamoja kwa kujifunza na kuchukua hatua stahiki.

‘Andika wosia sasa, maadam unaishi leo’

Kumbuka ‘kutokujua sheria si utetezi iwapo utatenda kosa lolote’ tafuta maarifa sahihi ya kisheria yakusaidie kufanya maamuzi sahihi kila siku.

Muhimu

Ikiwa una maswali au kuna eneo la kisheria ungependa kupata ufafanuzi basi nafasi ni yako na ndio msingi wa mtandao huu wa Uliza Sheria. Wasiliana nami na kuuliza maswali mbalimbali ili tuyachambue kwenye makala zijazo kwa njia ya e mail zakejr@gmail.com namba ya simu watsup 0713 888 040 na kwa sms .

‘Usikwame kwenye tatizo lolote la kisheria wakati unayo nafasi ya kuuliza, uliza sheria uoneshwe njia’

Nakutakia siku njema sana ndugu yangu.

Wako

Isaack Zake, Wakili

2 replies
  1. Log Me In
    Log Me In says:

    First off I want to say wonderful blog! I had a quick question which I’d
    like to ask if you do not mind. I was curious to know
    how you center yourself and clear your mind prior to
    writing. I have had a tough time clearing my mind in getting
    my ideas out. I truly do enjoy writing but it just seems like the first 10
    to 15 minutes tend to be lost just trying to figure out how to
    begin. Any recommendations or hints? Appreciate it!

    • ulizasheria
      ulizasheria says:

      Thank you for your comment on our blog.
      There is no special hints towards the capacity to write or figure out what to write. Sometimes I find very difficult to write but there are rules I have been meditating and repeating each day in my mind to form an attitude for which is a driving force no matter I feel to write or not. I would share with you.

      1. I recognise that the ability to write or compose message is my talent- it is God given gift
      2. I have formed a desire to write each day no matter what as long as I am in good health and alive. there is no excuse to that determination.
      3. I have given my self a duty to write as a service to human kind because I know through my writing I will save human kind to commit such errors which can cost lives or terms in prison since knowledge of law is inevitable, nothing can take place of law.
      4. Be Special, value yourself and the content you want to share because there is no one like you in this planet earth, so if you don’t do it no one will do.
      5. It is an investment of greater value, the history remember more those who put their thought into writing than those who speak, or do something. Do it don’t wait because the generation to follow will remember you for the contribution you will make.

      Karibu sana

Comments are closed.